Advertisement

Responsive Advertisement

Mvurugiko wa Hormon. Hormon im,balance.

 

Mvurugiko wa Hormon.
Hormon im,balance.

Dr_Ally_Herbalist✓.

Mvurugiko wa homoni za mwanamke ni kitendo cha kuongezeka au kupungua kwa vichochezi katika mwili wa mwanamke pale anapo pata hedhi, hivyo kufanya mwili kubadilika.

Mvurugiko huo huathiri kila mwanamke kwa zaidi ya 80%.

Asilimia  kubwa ya wanawake mabadiliko huanza kati ya miaka 40 na 50, lakini pia kukosekana  kwa usawa wa homoni huweza kuonekana mapema zaidi, kuanzia miaka 14.

Mabadiliko haya asilia hutokea wakati wa balehe, hedhi, ujauzito, kabla na baada ya ukomo wa hedhi.

Mvurugiko wa homoni kwa mwanamke huweza kuchangiwa kutokuwepo na usawa katika homoni za Estrogen na Progesterone.

Kupungua au kuzidi kwa homoni hizi hupelekea mvurugiko  wa homoni kwa mwanamke.

SABABU ZA MVURUGIKO WA HOMONI.

Mvurugiko wa homoninitatizo linalo
wakumba wanawake wengi kwa sasa.

Hii ni kutokana na maisha wanayoishi, elimu finyu waliyonayo juu ya afya zao na kutokula kulingana na makundi ya damu.

Vyanzo vya kuvurugika kwa homoni.

Uwepo wa sumu mwilini.

Unbalanced Lifestyle.
[mfumo mbovu wa maisha]

Umri ukienda sana.

Kukoma kwa hedhi.

Kutofanya mazoezi, na kutokulala masaa yanayostahili kwa siku.

Uzito mkubwa.

Mabadiliko ya mazingira au hali ya hewa.

Msongo wa mawazo.

Upungufu wa lishe mwilini.

Matumizi ya  njia za kisasa za uzazi wa mpango.

Utoaji wa mimba.

Upungufu au ongezeko la homoni ya progesterone na Estrogen.

Ongezeko la homoni ya Androgen [Kuota ndevu, sauti kama mwanaume]

DALILI ZA MVURUGIKO WA HOMONI.

Mfumo wa homoni ni muhimu sana kwa afya ya ubongo na mili yetu.

Husaidia kuzuia magonjwa yasiyo ambukizi kadri umri unavyo songa mbele.

Baadhi ya dalili zinazoweza kuonekana kwa mtu mwenye changamoto ya mvurugiko wa homoni ni Hizi hapa👇.

Ukavu ukeni.

Maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Kutoa jasho lingi nyakati za usiku.

Maumivu chini ya kitovu wakati wa hedhi.

Upungufu wa hamu ya tendo la ndoa.

Mabadiliko ya siku za hedhi na kupata hedhi kwa muda mrefu unaozidi siku 7.
[heavy bleeding, au kujaza pedi moja kwa saa moja].

Kukosa hedhi kwa muda mrefu, na kutoa damu yenye mabonge mabonge wakati wa hedhi.

Uchovu wa mara kwa mara.

Hasira za mara kwa mara.

Kukosa usingizi.

Homa za usiku na Kizunguzungu cha mara kwa mara.

Mzio wa vyakula (Allergie), kuchagua chagua vyakula.

Ongezeko la tumbo na nyama uzembe.

Kuharibika kwa ngozi (chunusi, vipele n.k).

Maumivu ya Mgongo na Kiuno.

Upungufu wa nywele  kichwani.

Kusahau sana [kukosa kumbukumbu].

Kupata hedhi wakati wa ujauzito [progesterone ikiwa imezidi].

Kutokupata hedhi [balehe] hadi umri wa miaka 20 na kuendelea.

Mwili kutokukua, kuonekana kama binti mdogo, na kutokukua kwa via vya uzazi.

Msongo wa mawazo na kukosa kujiamini.

Kusinyaa na kupauka kwa ngozi wakati wa siku za hedhi na wakati wa utumiaji wa njia za uzazi wa mpango.

Maumivu ya kichwa mara kwa mara.

Kuwa na tabia ya hamaki [kukosa utulivu].

Kutokupata choo kwa wakati.

MADHARA YA MVURUGIKO WA HOMONI.

Kutoshika ujauzito kwa muda mrefu.

Mimba kuharibika mara kwa mara.

Kukosa mtoto au Ugumba.

Maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Kuwa na tabia na maumbile ya kiume.

U.T.I [Urinary Tract Infection] ya mara kwa mara.

Kuzeeka mapema.

Kuziba kwa mirija ya uzazi.

Saratani.

Uvimbe kwenye Mji wa Kizazi wa mwanamke[Fibroids and Cysts].

SULUHISHO.

Tibu changamoto zote zinazohusu Afya yako,ili kuepuka Magonjwa nyemelezi.

Kwa ushauri Na Tiba Asili kabisa.

Wasiliana hapa👉0746382080

Post a Comment

0 Comments