Advertisement

Responsive Advertisement

Tatizo la Ganzi Miguuni na Mikono.


[Peripherial Neuropathy].

Tatizo la Ganzi Miguuni na Mikono.



Dr_Ally_Herbalist.

Peripherial neophathy Ni nini.

Huu Ni ugonjwa unaotokea pale neva za kwenye maeneo ya pembezoni mwa mwili hasa miguu na mikono kushindwa kufanya kazi kutokana na kupata majeraha.

Kujeruhiwa kwa neva kunasababisha mwili kutumwa kwa taarifa ya maumivu wakati hakuna maumivu, au kutotuma taarifa ya maumivu wakati kuna kitu kinachokuumiza.

Neva hizi zinaweza kujeruhiwa kutokana na Mambo yafuatayo.

Ajali.
Kuumwa magonjwa kwa Muda Mrefu.
Kupata maambukizi ya Magonjwa mbalimbali,  Au kurithi.

Dalili za Tatizo la Ganzi kwenye Miguu na Mikono.

Kutetemeka kwa mikono na miguu.
Kupata hisia kama umevaa kitu cha kubana kwenye mikono au miguu.

Kuangusha vitu mara kwa mara kutoka kwenye mikono.
Ngozi kuwa nyembamba.
Kushuka kwa shinikizo la damu.
Kupungua uwezo wa tendo la ndoa hasa kwa wanaume.
Tumbo kujaa gesi na kukosa choo.
Kuharisha na kutokwa na jasho lingi.

Nini Kinachosababisha Ganzi kwenye Miguu na Mikono.

Watu ambao familia zao zina historia ya kuugua tatizo hili wapo kwenye hatari kubwa ya wao kuugua tatizo hili kutokana na kurithi vinasaba.

Sababu zingine ni kama zifuatazo.

Magonjwa Kama Kisukari.

Kisukari ni ugonjwa unaoongoza kwa kuathiri neva za fahamu na kisha kupelekea mwili kuwa na ganzi kwenye mikono au miguu.

Kisukari husababisha kujeruhiwa kwa neva kutokana na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kutodhibitiwa.

Magonjwa mengine yanayoweza kujeruhi neva za fahamu na hivyo kupelekea ganzi miguuni na mikononi.

Magonjwa ya Figo.

Figo zisipofanya kazi vizuri hupelekea kiwango kikubwa cha sumu kujikusanya mwilini na kuathiri neva.

Kupungua uwezo wa tezi ya thyroid.

[Hypothyroidsm) kunapelekea mwili kuhifadhi maji kwenye eneo linalozunguka neva.

Upungufu wa vitamin E, B-1, B-6 na B-12 ambazo ni vitamini muhimu katika kuimarisha afya ya neva.

Mambo Mengine ambayo Ni chanzo.

Ajali.

Ajali ni moja ya sababu kubwa inayopelekea kuathirika kwa neva.

Ajali hizi ni pamoja na ajali za magari, kuanguka au kuvunjika kwa viungo.

Pombe na Sumu.

Pombe hupelekea kuchelewa kwa taarifa zinazosafirishwa na kuleta athari kwenye neva.

Watumiaji wa pombe waliokithiri wapo kwenye hatari zaidi ya kuugua ganzi kwenye miguu na mikono.

Watu wanaofanya kazi kwenye maeneo ya sumu na kemikali mfano sumu za kuulia wadudu, wanaweza kuugua tatizo hili la kupata ganzi ya mikono na miguu.

Maambukizi na Magonjwa ya Kinga.

Baadhi ya bateria na virusi wanaweza kushambulia neva.

Wagonjwa wa Ukimwi pamoja na wagonjwa wa tetekuwanga na mkanda wa jeshi wapo kwenye hatari ya kuugua tatizo hili la ganzi.

Matumizi ya Dawa kwa muda mrefu.

Matumizi ya baadhi ya dawa yanaweza kusababisha kuathirika kwa neva.

Mfano Kama hizi hapa👇.

Dawa za kutibu kifafa.
Antibiotics.
Baadhi ya dawa kwa ajili ya presha.
Dawa kwa ajili ya saratani.

Nini cha kufanya kwa Mgonjwa wa ganzi.

Moja ni kurekebisha tabia na mazingira yanayosababisha kama kisukari, ulevi na mazingira yenye kemikali.

Mazingira, tabia na Makundi yaliyopo kwenye Hatari zaidi kuugua Ganzi.

Kisukari.
Matumizi ya pombe kwa muda mrefu.
Kupungukiwa na Vitamin hasa Vitamin B.
Wagonjwa Ukimwi, mkanda wa jeshi na tetekuwanga.

Magonjwa ya kinga kushambulia tishu [autoimmune diseases].

Kuwa na magonjwa ya figo, ini na tezi ya thyroid.

Sababu nyingine za kupatwa na ganzi.

Matumizi ya Maji kwa wingi, Yaani kuyakanyaga, au kuyashika kwa kipindi kilefu nayo husababisha ganzi ya miguu na Mikono.

Familia zenye historia ya kuugua ganzi.

Zingatia maisha ya kiafya kama; kula lishe yenye matunda, mboga ili kuimarisha afya ya neva.

Tumia vyakula veynye vitamin B-12 kwa wingi kama nyama, samaki, mayai.

Fanya mazoezi ya viungo mara kwa mara.

Weka ratiba ya kufanya mazoezi mara 4 kwa week, Nusu saa kwa siku.

Epuka mazingira yanayoweza kujeruhi neva kama .

Kufanya kazi kwenye mazingira yenye kemikali kwa muda mrefu, kuvuta sigara na matumizi ya pombe kupita kiasi.

𝐊𝐰𝐚 𝐓𝐢𝐛𝐚 𝐁𝐨𝐫𝐚 𝐍𝐚 𝐔𝐬𝐡𝐚𝐮𝐫𝐢.
𝐌𝐚𝐰𝐚𝐬𝐢𝐥𝐢𝐚𝐧𝐨 📲0746382080

Post a Comment

0 Comments