Advertisement

Responsive Advertisement

Pelvic Infalammatory Disease [PID].

Pelvic Infalammatory Disease [PID].



   Dr_Ally_Herbalist.

P.I.D Ni Nini.

[P.I.D], ni maambukizi yanayotokea kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke.

P.I.D hutokea pale bakteria waenezwao kwa ngono wanaposambaa kutoka kwenye uke [vagina] hadi kwenye nyumba ya uzazi [uterus], mirija ya uzazi [fallopian tubes] na ovari.

Dalili za P.I.D huweza kuwa ni ngumu kueleweka.

Baadhi ya wanawake hawaoni dalili zo zote.

Kwa maana hiyo, unaweza usihisi cho chote hadi pale utakaposhindwa kupata ujauzito au hadi utakapoanza kupata maumivu ya kiuno.

Dalili Za PID.

P.I.D inaweza isilete dalili zo zote mbaya na ndogo zikitokea zinaweza kuwa ngumu kuzigundua.

Baadhi ya wanawake hawapati dalili zo zote.

Pale zinapojitokeza, zinaweza kuwa Kama ifuatavyo.

Maumivu – yanaweza kuwa madogo au makali – maeneo ya chini ya tumbo au nyonga.

Uchafu usio wa kawaida au mzito ambao unaweza kuwa na harufu mbaya.

Kutokwa damu kusiko kwa kawaida, hasa wakati wa tendo la ndoa, au katikati ya siku.

Maumivu wakati wa kujamiiana.
Homa, wakati mwingine kusikia baridi.
Maumivu wakati wa haja ndogo.

Haja ndogo ya mara kwa mara au haja ndogo kutoka kwa shida.

Chanzo Cha P.I.D

Kuna bakteria wa aina nyingi wanaoweza kusababisha PID, lakini maambukizi ya gonorrhea na chlamydia ndiyo yanayoonekana zaidi.

Bakteria hao huambukiza wakati tendo la ndoa linapofanyika bila ya kutumia kinga.

Aghalabu, bakteria hawa huingia kwenye viungo ya uzazi vya mwanamke pale ulinzi wa kwenye shingo ya kizazi [cervix] unapovurugwa.

Hii inaweza kutokea mathalani, wakati wa hedhi na baada ya kuzaa, mimba kuharibika au kutoka mimba.

Mara chache bakteria huweza kujipenyeza wakati kifaa cho chote cha tiba kinapoingizwa kwenye nyumba ya uzazi.

Mazingira Hatarishi.

Kuna vipengele ambavyo huweza kukuweka kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata PID.

Vipengele Hivyo Ni hivi hapa 👇.

Kuwa mwanamke uliye chini ya miaka 25 unayeshiriki ngono.

Kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja.

Kuwa na mahusiano na mpenzi mwenye wapenzi zaidi ya mmoja.

Kufanya mapenzi bila kinga.
Kujisafisha na maji mara kwa mara

Kuwa uliwahi kupata P.I.D kabla au magonjwa mengine ya ngono.

Madhara Yatokanayo na P.I.D

P.I.D ambayo haikupata tiba inaweza kusababisha makovu na vifuko vyenye maji yenye wadudu kwenye mkondo wa njia ya uzazi ya mwanamke.

Vitu hivi vinaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye viungo vya uzazi.

Madhara yanayoweza kutokea ni haya hapa.

Mimba nje ya mirija [ectopic pregnancy].

P.I.D ndiyo sababu kubwa ya mimba kutunga nje ya kizazi.

Mimba huweza kutunga nje ya kizazi endapo P.I.D imesababisha makovu ndani ya mirija ya uzazi.

Makovu haya husababisha yai lililopevushwa kushindwa kusafiri ndani ya mirija ya uzazi kuelekea kwenye nyumba ya uzazi.

Badala yake yai hunata ndani ya mirija ya uzazi .

Mimba nje ya kizazi husababisha utokaji wa damu usio wa kawaida unaoweza kukatisha maisha ya mwanamke.

Ugumba.

Uharibifu wa viungo vya uzazi huweza kusababisha ugumba – kushindwa kupata ujauzito.

Kadiri unavyozidi kupata P.I.D mara nyingi zaidi, ndivyo hatari ya ugumba inavyozidi.

Kuchelewa kupata tiba ya P.I.D kunaongeza hatari ya ugumba.

Maumivu sugu ya nyonga.

P.I.D inaweza kusababisha maumivu ya nyonga yanayoweza kudumu kwa miaka mingi.

Makovu ndani ya mirija ya uzazi na viungo vingine vya uzazi huweza kuleta maumivu wakati wa kujamiiana na wakati yai linadodondoshwa [ovulation].

Tubo-ovarian abscess.

P.I.D huweza kusababisha kutunga kwa usaha na kufanya majipu ndani ya njia ya uzazi.

Mara nyingi majibu haya hutokea ndani ya mirija ya uzazi na ovari, ingawa huweza kuota ndani ya nyumba ya uzazi na shingo ya kizazi.

Kama tiba haitatolewa, unaweza kupata maambukizi hatarishi kwa maisha.

Tiba Ya P.I.D

Tiba ya mara moja kwa kutumia dawa itaondoa maambukizi yaliyosababisha PID, Lakini, hakuna njia ya kukarabati makovu au uharibifu kwenye njia ya viungo vya uzazi uliotokana na PID.

Tiba ya PID yaweza kuwa,  Antibiotics.

Daktari atakuandikia dawa inayoendana na chanzo cha tatizo lako, Utasubiri siku kama tatu kuona kama dawa ulizopewa zinafanya kazi.

Ushauri wa bure.

Kumtibu Mwenza wako, Kuzuia maambukizi, yafaa mwenzi wako afanyiwe uchunguzi na atibiwe pia.

Kuacha kushiriki ngono kwa muda.

Acha kushiriki ngono hadi utakapomaliza tiba na kuona kuwa umepona.

Ukurasa wetu mwingine tutauzungumzia ugonjwa wa kuziba kwa mirija ya uzazi.

Usisite kutoa maoni kuhusu ukurasa huu au kuuliza maswali uliyo nayo.

𝐊𝐰𝐚 𝐓𝐢𝐛𝐚 𝐁𝐨𝐫𝐚 𝐍𝐚 𝐔𝐬𝐡𝐚𝐮𝐫𝐢.
𝐌𝐚𝐰𝐚𝐬𝐢𝐥𝐢𝐚𝐧𝐨 📲0746382080

Post a Comment

0 Comments