Advertisement

Responsive Advertisement

Chanzo cha Maumivu Ya Chuchu kwa wanawake na jinsi ya kuyaepuka.

Chanzo cha Maumivu Ya Chuchu kwa wanawake na jinsi ya kuyaepuka.



Dr_Ally_Herbalist.

Maumivu ya chuchu.

Chuchu ni eneo la matiti ambalo linakuwa na msisimko sana ambalo laweza kuuma kwa sababu mbalimbali.

Nguo za kubana, vipele na pia maambukizi ya bacteria au fangasi yanaweza kufanya ngozi kututumka na hivyo kuleta maumivu ya chuchu.

Kwa wanawake wengi  chuchu zao huvimba hasa wakati wa hedhi, mimba na kipindi cha kunyonyesha.

Wanawake wengi pia hupata hofu pale wakijiskia maumivu ya chuchu na kuhisi kwamba pengine wameanza kupata saratani ya matiti.

Sababu za Maumivu ya Matiti.

Nguo isiyokaa vizuri, Uvaaji wa bra au shati ambalo halijakaza vizuri hupelekea msuguano na chuchu kila mara, pengine wakati wa kutembea ama kukimbia.

Msuguano huo husababisha chuchu kuvimba na hata kutoa damu. 

Kuepuka tatizo hili hakikisha unavaa topu na sidiria zinazokutosha vizuri, isiwe kubwa kuliko na isiwe ndogo sana.

Matatizo ya ngozi.

Magonjwa ya ngozi kama pumu ya ngozi ama fangasi ya ngozi ni chanzo cha kuvimba na vilevile maumivu ya chuchu, onana na daktari kama una ugonjwa wowote wa ngozi upate tiba mapema.

Hedhi.

Kuvimba na maumivu ya chuchu inaweza kuwa ni kiashiria cha hedhi kukaribia.

Hedhi inapokaribia homoni ya estrogeni huzalishwa kwa wingi na kupelekea chuchu kuvimba na kuuma.

Maumivu haya  huisha baada ya hedhi kupita .

Mimba, [Ujauzito].

Wakati wa mimba kunatokea mabadiliko makubwa ya vichocheo/homoni na hivyo kufanya matiti kuwa laini, kuvimba  na kuuma.

Chuchu huanza kutoamaji maji kama maziwa kadri unavokaribia kujifungua.

Kama maumivu ni makali sana, ongea na daktari wako akupatie vidonge salama vya kupunguza maumivu.

Kunyonyesha.

Chuchu huuma pale mtoto anapovuta titi wakati wa kunyonya, maumivu haya yanaweza kuwa kama umechomwa sindano kwa mbali ila yataisha ndani ya muda mfupi.

Jinsi ya Kupunguza Maumivu ya Chuchu wakati unanyonyesha.

Kabla hujanyonyesha binya titi upate maziwa kidogo kisha yapake eneo la chuchu.

Unaweza kupaka mafuta salama kwa mtoto kwenye eneo la titi, ongea na daktari kupata pendezo la mafuta ya kutumia.

Hakikisha chuchu zako zinakauka kila unapomaliza kunyonyesha na ubadili sponge ya kunyonya matiti mara kwa mara.

Vaa sidiria nzuri ya pamba kwa ajili ya kunyonyesha, hakikisha inakutosha vizuri na haisuguani na chuchu zako.

Jaribu njia na mikao mbalimbali ya kunyonyesha mpaka upate mkao unaokufaa na usiokuumiza.

Sababu zingine na Maumivu ya Matiti yako ni pamoja na haya hapa.

Maambukizi.

Mambukizi yaweza kuwa chanzo cha maumivu yako ya chuchu.
Mfano: maambukizi ya kwenye mrija wa maziwa kitaalamu [mastitis] ambayo husababishwa na bacteria kukua na kuathiri mshipa wa maziwa ulioziba ni chanzo kikubwa cha maumivu kwa wanawake wengi wanaonyonyesha.

Hakikisha unatumia dozi nzima utakayoandikiwa na daktari kutibu changamoto hii.

Saratani ya matiti.

Kama maumivu yako ya chuchu yanaambatana na dalili zingine.

Mfano.

Chuchu kutengeneza shimo baada ya kubinya, kutokwa na majimaji yasiyo maziwa, kuvimba chini ya kwapa, chuchu kuwa nyekundu na kutengeneza magamba.

Ukiona dalili hizi nenda hospitali haraka daktari akufanyie vipimo kujua kama una saratani ili uanze tiba mapema.

𝐊𝐰𝐚 𝐓𝐢𝐛𝐚 𝐁𝐨𝐫𝐚 𝐍𝐚 𝐔𝐬𝐡𝐚𝐮𝐫𝐢.
𝐌𝐚𝐰𝐚𝐬𝐢𝐥𝐢𝐚𝐧𝐨 📲0746382080

Post a Comment

0 Comments