Ujuwe Ugonjwa wa U.T.I na Tiba zake.
Dr_Ally_Herbalist.
Maana ya U.T.I
U.T.I ni kifupi cha maneno ya kiingereza [Urinary tract infections"],ni maambukizi ya bakteria katika njia ya mkojo.
Husababishwa na bacteria aina ya clamydia tracomatis.
Ni moja ya ugonjwa unaowakumba sana wanawake kwa sehemu kubwa ingawa hata wanaume pia wanapatwa na ugonjwa huu.
Chanzo cha Tatizo.
Kushikilia mkojo kwa muda mrefu.
Kukojoa kwenye maji machafu.
Mawe kwenye figo.
Kuongezeka ukubwa wa kibofu cha mkojo.
Upungufu wa maji mwilini.
Ajari katika uti wa mgongo.
Maji maji na uchafu katika sehemu za siri.
Kufanya ngono na muathilika wa U.T.I
Kujisaidia sana kwenye vyoo vya uma.
Dalili za ugonjwa
kujisikia homa kali.
Kuhisi baridi kali.
Maumivu nyuma ya mgongo
Kukojoa mara kwa mara
Mikojo kukutoka pasipo kutaka
Harufu nzito au mbaya ya mkojo.
Hali ya kusikia kuungua wakati wa kukojoa.
Kupatwa ghafla na hitaji la kutaka kukojoa.
Mkojo kutoka wa rangi ya njano.
Maumivu kwenye kibofu cha mkojo na urethra.
Damu kutoka pamoja na mkojo.
Tiba ya Tatizo.
1. Kitunguu swaumu.
Ni mojawapo ya tiba mbadala ya kutibu U.T.I. Ni dawa nzuri dhidi ya bakteria na virusi
Jinsi ya kutumia.
Chukuwa kitunguu swaumu kimoja na ukigawe upate punje 6, kisha kikatekate vipande vidogo vidogo na kisu kisha meza kama unavyomeza dawa nyingine yoyote na maji glass 2 kila unapoenda kulala.
2. Unga wa mlonge.
Tumia kijiko kidogo kimoja cha chai ndani ya uji, au ndani ya juisi ya matunda kikombe kimoja (robo lita), au katika maji ya uvuguvugu glass 1, kutwa mara 1, kwa siku7.
3. Mshubili [Aloe vera].
Chukua mshubiri [Aloe-vera],vijiko vikubwa viwili, changanya na maji ya kawaida ili kupata robo lita, changanya vizuri mchanganyiko huu na unywe kutwa mara 1 kwa siku 3.
Unaweza kuongeza asali ndani yake vijiko vikubwa vitatu ili kupunguza ukali wa dawa hii.
𝐊𝐰𝐚 𝐓𝐢𝐛𝐚 𝐁𝐨𝐫𝐚 𝐍𝐚 𝐔𝐬𝐡𝐚𝐮𝐫𝐢.
0 Comments